• HABARI MPYA

  Jumapili, Oktoba 20, 2019

  SAMATTA ‘AWAKOSAKOSA’ STANDARD LIEGE LIGI YA UBELGIJI, KRC GENK YALAMBWA 1-0 UGENINI

  Na Mwandishi Wetu, LIEGE
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania jana amecheza mechi ya kwanza baada ya kuoa, bahati mbaya timu yake, KRC Genk imechapwa 1-0 na Standard Liege katika mchezo wa ugenini wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji Uwanja wa Maurice Dufrasne mjini Liege.
  Bao pekee lililoizamisha KRC Genk jana lilifungwa na kiungo Mbelgiji, Samuel Bastien dakika ya 84 akimalizia pasi ya beki Mcameroon, Ngoran Suiru Fai Collins.
  Na kwa matokeo hayo, mabingwa hao watetezi wanabaki na pointi zao 16 katika mchezo wa 10, mwenendo ambao unaanza kuleta shaka kama wataweza kubakiza Kombe Genk.

  Samatta wiki iliyopita alikuwa Dar es Salaam kwa ajili ya kufunga ndoa na mpenzi wake, jana hakika hakuwa katika ubora wake na alipoteza nafasi nzuri ya kufunga kipindi cha kwanza. 
  Samatta jana alicheza mechi 168 kwenye mashindano yote tangu ajiunge na KRC Genk Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) akiwa amefunga mabao 68 jumla.
  Katika ligi ya Ubelgiji pekee amecheza mechi 132 na kufunga mabao 52, kwenye Kombe la Ubelgiji amecheza mechi tisa na kufunga mabao mawili, katika Super Cup mechi moja, Ligi ya Mabingwa Ulaya mechi mbili na bao moja na Europa League mechi 24 na mabao 14.
  Kikosi cha Standard Liege kilikuwa: Bodart, Vanheusden, Cimirot, Amallah/Carcela dk72, Fai, Lestienne/Vojvoda dk92, Gavory, Avenatti/Oulare dk81, Bastien, Laifis na Mpoku.
  KRC Genk: Coucke, Mæhle, Dewaest, Lucumi, Uronen, Berge, Heynen/Onuachu dk87, Hagi/Hrosovsky dk60, Ito/Ndongala dk81, Bongonda na Samatta.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SAMATTA ‘AWAKOSAKOSA’ STANDARD LIEGE LIGI YA UBELGIJI, KRC GENK YALAMBWA 1-0 UGENINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top