• HABARI MPYA

    Tuesday, October 29, 2019

    EBITOKE AFURAHISHWA NA MAHUSIANO MAZURI YA KIMTANDAO BAINA YA TANZANIA NA CHINA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    MSANII wa vichekesho hapa nchini Anastazia Exavery maarufu kwa jina la 'Ebitoke', amekoshwa na mahusiano mazuri ya kimtandao baina ya Tanzania na China.
    Ebitoke ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa pande hizo mbili Tanzania na China na yeye akiwa mmoja wa wageni wenye ushuhuda wa mitandao ya kijamii.
    Msanii huyo alisema, anaimani muunganiko huu wa nchi zote mbili utakuwa ni tija kubwa kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii. 
    "Mitandao ya kijamii ni kitu kikubwa sana kwani Mimi ni shahidi mkubwa sana katika hilo, kwani nimepata umaarufu mkubwa kupitia mitandao hiyo ya kijamii mpaka sasa nina wafuasi zaidi ya mil 2 naenda mil 3,"amesema.

    Mkutano huo ulioandaliwa na startimes umekuwa na manufaa makubwa kwa washiriki kwani wengi wao walikiri mitandao hiyo ya jamii ni moja ya sehemu za kumuinua mtu kwa namna moja ama nyingine.
    Nae Zhau Hui kutoka China alisema, wao wamefarijika sana na kufurahi kuendeleza muunganiko huo ambao ulianza miaka mingi iliyopita na Sasa ukikua zaidi kupitia mitandao ya kijamii.
    "Sisi China muungano huu na Tanzania ni kubadilishana utamaduni wa kimitandao ambao kwa Sasa ndio umepiga hatua kubwa,"alisema.
    Nae Samia Mussa ambaye ni moja ya waingiza sauti katika tamthilia mbalimbali za kichina, alikiri ushirikiano huu utazaa matunda na utakuwa moja ya sehemu kubwa ya hata wao kutangaza kazi zao na kukulikana zaidi.
    Alisema mitandao ya kijamii kwa Sasa imesambaa sana na watu wengi wanaitumia mitandao hii ya kijamii hivyo ni moja ya mafanikio ya kukivunia katika kupiga hatua na wao kuonyesha kazi zao zaidi ambazo zinawapa pesa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: EBITOKE AFURAHISHWA NA MAHUSIANO MAZURI YA KIMTANDAO BAINA YA TANZANIA NA CHINA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top