• HABARI MPYA

  Jumapili, Oktoba 27, 2019

  SAMATTA ATOLEWA DAKIKA ZA MWISHONI GENK YAICHAPA 1-0 CERCLE BRUGGE LIGI YA UBELGIJI

  Na Mwandishi Wetu, GENK
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta jana amecheza kwa dakika 80 timu yake, KRC Genk ikiibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Cercle Brugge katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk.
  Samatta alitolewa dakika ya 80, nafasi yake ikichukuliwa na kiungo Mromania, Ianis Hagi dakika ya 80 na wakati huo tayari Genk inagongoza 1-0, bao lililofungwa na beki Mbelgij, Sébastien Dewaest.
  Kwa ushindi huo, Genk inafikisha pointi 19 baada ya kucheza mechi 11, ikizidiwa pointi sava na vinara, Club Brugge wenye pointi 26, wakifuatiwa na Standard Liège pointi 23.  
  Samatta jana amecheza mechi ya ya 170 jumla kwenye mashindano yote tangu ajiunge na KRC Genk Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) akiwa amefunga mabao 68.
  Katika ligi ya Ubelgiji pekee amecheza mechi 133 na kufunga mabao 52, kwenye Kombe la Ubelgiji amecheza mechi tisa na kufunga mabao mawili, katika Super Cup mechi moja, Europa League mechi 24 na mabao 14 na Ligi ya Mabingwa Ulaya tatu tu akiwa amefunga bao moja.
  Kikosi cha KRC Genk kilikuwa: Coucke, Maehle/Berge dk54, Dewaest, Cuesta, De Norre, Wouters, Hrosovsky, Ito, Ndongala/Bongonda dk72, Samatta/Hagi dk80 na Onuachu.
  Cercle Bruges; Hubert, Serrano/Deman dk64, Ueda, Hazard, Peeters, Panzo, Dabila, Dekuyper/Somers dk79, Gory, Donsah na Biancone/Hoggas dk92.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SAMATTA ATOLEWA DAKIKA ZA MWISHONI GENK YAICHAPA 1-0 CERCLE BRUGGE LIGI YA UBELGIJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top