• HABARI MPYA

  Jumapili, Oktoba 20, 2019

  STARS ILIYOWEKA KAMBI UJERUMANI IKAENDA KUVURUNDA CHALLENGE

  WACHEZAJI wa kikosi cha Tanzania Bara wakiwa mjini Berlin nchini Ujerumani Oktoba mwaka 1987 walipoweka kambi kujiandaa na michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge iliyofanyika nchini Ethiopia mwaka 1987. Kutoka kulia waliosimama ni Abeid Mziba, Mavumbi Omar (marehemu), Khalfan Ngassa, Michael Kidilu, Hussein Mwakuruzo, John Makelele na Michael John.
  Walioketi kutoka kulia ni Sanifu Lazaro, Raphael Paul (marehemu), Edgar Fongo, Said John, Yassin Napili, Issa Athumani (marehemu) na waliopiga magoti ni makipa John Bosco (kulia) na Sahau Kambi (kushoto). 
  Pamoja na kambi ya Ujerumani, Kilimanjaro Stars ilitolewa mapema baada ya sare 0-0 na wenyeji, Ethiopia kabla ya kufungwa mechi mbili zilizofuata 3-2 na Kenya na 2-0 na Zanzibar, hivyo kushika mkia Kundi A.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: STARS ILIYOWEKA KAMBI UJERUMANI IKAENDA KUVURUNDA CHALLENGE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top