• HABARI MPYA

  Jumanne, Septemba 03, 2019

  TAIFA STARS WALIVYOONDOKA LEO DAR KUIFUATA BURUNDI KWA MECHI YA KUFUZU KOMBE LA DUNIA KESHO

  Beki Kelvin Yondan akiwaongoza wachezaji wenzake wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kuingia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) mjini Dar es Salaam kwa safari ya Bujumbura nchini Burundi leo asubuhi
  Taifa Stars inakwenda Bujumbura kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania tiketi ya Fainali za Kombe la Dunia Qatar 2022
  Kipa Juma Kaseja akiingia JNIA kwenda Bujumbura kwa ajili ya mchezo ambao utafanyika kesho
  Timu hizo zitarudiana Jumapili Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam na mshindi wa jumla atapangwa katika moja ya makundi 10 kuanza rasmi mbio za Qatar 2022
  Kiungo Mohammed Issa 'Banka' akiingia JNIA leo asubuhi tayari kwa safari
  Kipa wa Simba SC, Beno Kakolanya akiwaongoza wenzake kuingia JNIA
  Hapa ni wakati wakipata mlo wa asubuhi kabla ya safari yao  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TAIFA STARS WALIVYOONDOKA LEO DAR KUIFUATA BURUNDI KWA MECHI YA KUFUZU KOMBE LA DUNIA KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top