• HABARI MPYA

  Jumatatu, Septemba 02, 2019

  AZAM FC YAICHAPA TRANSIT CAMP 3-1 MECHI YA KIRAFIKI KUJIANDAA KUIVAA POLISI LIGI KUU

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KATIKA kujiandaa na mchezo wake ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Azam FC jana ilicheza mechi ya kujipima nguvu dhidi ya Transit Camp ya Daraja la Kwanza na kuibuka na ushindi wa 3-1 Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.
  Ilikuwa siku nzuri kwa mshambuliaji Mzimbabwe, Donald Dombo Ngoma aliyefunga mabao mawili, huku lingine likifungwa na beki Mghana, Daniel Amoah. 
  Azam FC itacheza mechi yake ya pili ya Ligi Kuu Septemba 18 dhidi ya wenyeji, Polisi Tanzania Uwanja wa Ushirika mjini Moshi kufuatia kushinda1-0 dhidi ya KMC kwenye mchezo wake wa kwanza wiki iliyopita.

  Baada ya raundi moja tu ya kwanza, Ligi Kuu ya Tanzania Bara imesimama kwa sasa kupisha mechi za mchujo wa kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia Qatar mwaka 2022.
  Tanzania itasafiri kesho kwenda Bujumbura kwa ajili ya mchezo dhidi ya wenyei Int’hamba Murugamba Jumatano mjini Bujumbura kabla ya timu hizo kurudiana Jumapili wiki hii Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
  Mshindi wa jumla atafuzu kwenye hatua ya makundi 10, ambayo washindi wa kwanza watamenyana baina yao kupata wawakilishi watano wa Afrika kwenye fainali zijazo za Kombe la Dunia. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AZAM FC YAICHAPA TRANSIT CAMP 3-1 MECHI YA KIRAFIKI KUJIANDAA KUIVAA POLISI LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top