• HABARI MPYA

  Jumamosi, Septemba 28, 2019

  ALLIANCE FC YAZINDUKA NA KUWACHAPA SINGIDA UNITED 1-0 NAMFUA, RUVU NAYO YANG’ARA

  Na Mwandishi Wetuk SINGIDA
  TIMU ya Alliance FC imepata ushindi wa ugenini wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Singida United jioni ya leo Uwanja wa Namfua mjini Singida.
  Bao hilo pekee limefungwa na Sameer Vincent dakika ya 16 na kwa ushindi huo wa kwanza wa msimu katika mechi ya mechi nne, Alliance FC inafikisha pointi tano kufuatia sare mbili awali na kufungwa mchezo mmoja.
  Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Ruvu Shooting imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Polisi Tanzania bao pekee la Yassin Salum aliyejifunga dakika ya tano Uwanja wa Meja Isamuhyo, Mbweni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

  Nayo Mwadui FC imelazimishwa sare ya 1-1 na jirani zao, Mbao FC ya Mwanza Uwanja wa Mwadui Complex mjini Shinyanga. Gerald Mathias alianza kuifungia Mwadui FC dakika ya 58 kabla Chilo Mkama kuisawazishia Mbao FC dakika ya 90.
  Ligi Kuu ya Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea leo kwa mechi tano kupigwa kwenye viwanja tofauti, ikiwemo mabingwa watetezi, Simba SC kuwa wageni wa Biashara United Uwanja wa Karume mjini Musoma mkoani Mara.
  Lipuli FC watakuwa wenyeji wa Tanzania Prisons Uwanja wa Samora mjini Iringa, Mtibwa Sugar wanawakaribisha Mbeya City Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, Kagera Sugar wanawakaribisha JKT Tanzania Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba na KMC watakuwa wenyeji wa Ndanda FC Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ALLIANCE FC YAZINDUKA NA KUWACHAPA SINGIDA UNITED 1-0 NAMFUA, RUVU NAYO YANG’ARA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top