• HABARI MPYA

  Jumanne, Septemba 24, 2019

  TANZANIA BARA YATOA SARE 2-2 NA KENYA MICHUANO YA CECAFA CHALLENGE U20 UGANDA

  Na Mwandishi Wetu, JINJA
  TANZANIA Bara imetoa sare ya kufungana mabao 2-2 na Kenya katika mchezo wa Kundi B michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 20 Afrika Mashariki na Kati (CECAFA Challenge U20) leo mjini Jinja, Uganda.
  Mabao ya Tanzania Bara inayofundishwa na kocha wa Mtibwa Sugar ya Morogoro, Zubery Katwila yamefungwa na Andrew Albert Simchimba dakika ya 39 na Abdul Hamisi Suleiman dakika ya 56, wakati ya Kenya yamefungwa na Otieno Austine Odhiambo dakika ya 28 na Patrick Otieno dakika ya 52.
  kwa ushindi huo, Tanzania Bara inayofundishwa na Zubery Katwila ambaye pia ni kocha wa Mtibwa Sugar inafikisha pointi nne kufuatia kushinda 4-0 dhidi ya Ethiopia kwenye mchezo wa kwanza, siku ambayo Simchimba alifunga mabao matatu peke yake, linguine likifungwa na Kelvin Pius John.

  Ngorongoro Heroes itarudi uwanjani Jumanne Alhamisi kukamilisha mechi zake za Kundi B kwa kumenyana na ndugu zao, Zanzibar.
  Hatua ya Robo Fainali itafuatia Septemba 29, Nusu Fainali Okatoba 2 na Fainali ya michuano ya CECAFA Challenge U20 mwaka 2019 itapigwa Oktoba 5.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TANZANIA BARA YATOA SARE 2-2 NA KENYA MICHUANO YA CECAFA CHALLENGE U20 UGANDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top