• HABARI MPYA

  Alhamisi, Septemba 26, 2019

  TANZANIA BARA KUIVAA UGANDA ROBO FAINALI CHALLENGE U20 BAADA YA KUIPIGA ZENJI 5-0 LEO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Tanzania Bara itakutana na wenyeji, Uganda katika Robo Fainali ya michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 20 Afrika Mashariki na Kati (CECAFA Challenge U20) Jumapili kuanzia Saa 10:00 jioni mjini Gulu nchini humo.
  Hiyo ni baada ya leo kuwachapa 5-0 ndugu zao, Zanzibar katika mchezo wa mwisho wa Kundi B Uwanja wa Jinja nchini Uganda, chipukizi Kelvin Pius Jonh ‘Mbappe’ akifunga mabao matatu dakika za 51,87 na 90, mengine Lusajo Mwaikenda dakika ya tano na Novatus Dominic dakika ya 67.

  Tanzania Bara imepwwa uongozi wa Kundi B kwa sheria ya mchezo wa kiungwana kutokana na kuwa na kadi chache kuliko Kenya waliofungana nao kwa kila kitu.
  Robo Fainali nyingine ni kati ya Sudan na Sudan Kusini itakayochezwa Gulu pia kuanzia Saa 7:00 mchana, Burundi na Kenya Saa 7:00 mchana na Eritrea na Zanzibar Saa 10:00 jioni ambazo zote zitachezwa Njeru.
  Hatua ya Nusu Fainali itafuatia Okatoba 2 na Fainali ya michuano ya CECAFA Challenge U20 mwaka 2019 itapigwa Oktoba 5.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TANZANIA BARA KUIVAA UGANDA ROBO FAINALI CHALLENGE U20 BAADA YA KUIPIGA ZENJI 5-0 LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top