• HABARI MPYA

  Jumapili, Septemba 22, 2019

  AZAM FC YAWASILI MAPEMA ZIMBABWE TAYARI KUPINDUA MATOKEO DHIDI YA TRIANGLE UNITED JUMAMOSI

  Na Mwandishi Wetu, HARARE
  KIKOSI cha Azam FC kimeshawasili salama mjini Harare nchini Zimbabwe mchana huu, tayari kwa mchezo wa marudiano wa Raundi ya Pili ya kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji, Triangle United Jumamosi.
  Azam FC watahitaji ushindi wa ugenini wa kuanzia mabao 2-0 Jumamosi Uwanja wa Barbourfields mjini Bulawayo ili wasonge mbele, baada ya kufungwa 1-0 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam Septemba 15.
  Na msafara wa Azam FC uliowasili leo Harare, umefikia katika hoteli ya Cresta Lodge ulitarajiwa kuanza mazoezi leo jioni hadi Alhamisi itakaposafiri kwa barabara kwenda Bulawayo.

  Wachezaji wa Azam FC wakiwasili mjini Harare leo tayari kwa mechi ya marudiano na Triangle United Jumamosi

  Timu ipo chini ya Kocha Msaidizi, Iddi Nassor ‘Cheche’ kwa sababu kocha Mkuu, Mrundi Etienne Ndayiragijje yupo na timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ambayo leo inamenyana na Sudan kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) mwakani nchini Cameroon.
  Katika mchezo wa kwanza, bao pekee lililoizamisha Azam FC leo limefungwa na Ralph Kawondera dakika ya 35 akimalizia krosi iliyopigwa na Russel Madamombe, ingawa pamoja na kufungwa, Azam FC ilicheza vizuri na kutengeneza nafasi kadhaa nzuri, lakini tatizo kubwa lilikuwa kwenye umaliziaji.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AZAM FC YAWASILI MAPEMA ZIMBABWE TAYARI KUPINDUA MATOKEO DHIDI YA TRIANGLE UNITED JUMAMOSI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top