• HABARI MPYA

  Sunday, September 15, 2019

  TYSON FURY AKIMBIZWA HOSPITALI BAADA YA KUJERUHIWA ULINGONI

  Bondia Muingereza Tyson Fury akivuja damu baada ya kuchapwa ngumi kali na mpinzani wake, Msweden Otto Wallin katika pambano la uzito wa juu Alfajiri ya leo ukumbi wa T-Mobile Arena mjini Las Vegas, Marekani. Hata hivyo, Fury alishinda kwa pointi pambano hilo la raundi 10 na kuendeleza rekodi yake ya kushinda mapambano yake yote 30 ingawa baada ya mchezo huo alikimbizwa hospitali kwa matibabu na kushindwa kuzungumza na Waandishi wa Habari. Fury anatarajiwa kurejea ulingoni Februari 22 kwa pambano la marudiano na Deontay Wilder hapo hapo Vegas 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TYSON FURY AKIMBIZWA HOSPITALI BAADA YA KUJERUHIWA ULINGONI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top