• HABARI MPYA

  Sunday, September 15, 2019

  AZAM FC YACHAPWA 1-0 NYUMBANI NA TRIANGLE FC YA ZIMBABWE KOMBE LA SHIRIKISHO

  Na Saada Salim, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Azam FC imejiweka katika mazingira magumu kusonga mbele kwenye Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kufungwa 1-0 na wageni Triangle FC ya Zimbabwe katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Pili jioni ya leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam.
  Bao lililoizamisha Azam FC leo limefungwa na Ralph Kawondera dakika ya 35 akimalizia krosi iliyopigwa na Russel Madamombe.
  Pamoja na kufungwa, Azam FC ilicheza vizuri na kutengeneza nafasi kadhaa nzuri, lakini tatizo kubwa lilikuwa kwenye umaliziaji.

  Beki Mghana, Yakub Mohammed aliunganishai nje kidogo ya lango kwa kichwa kona iliyopigwa na mshambuliaji Mzambia, Obrey Chirwa dakika ya sita ambaye naye pia alikaribia kufunga dakika ya 13 kama si shuti lake kutoka nje kidogo. 
  Kipindi cha pili kocha Mrundi wa Azam FC, Etienne Ndayiragijje alitumia maarifa mapya kulazimisha matokeo mazuri nyumbani, ikiwemo kumuingiza na kumtoa mshambuliaji wa zamani wa Tenerife ya Hispania, SHaaban Iddi Chiliunda, lakini bado haikusaidia.
  Sasa Azam FC italazimika kwenda kushinda ugenini kwenye mchezo wa marudiano Septemba 28 Uwanja wa Barbourfields mjini Bulawayo. 
  Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Razak Abalora, Daniel Amoah, Yakubu Mohammed, Mvuyekure Emmanuel/Mudathir Yahya dk78, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Richard Ella D’jodi/ Shaaban Iddi Chilunda dk52/ Iddi Kipagwile dk71 Obrey Chirwa, Nico Wadada, Frank Domayo, Iddi Suleiman ‘Nado’ na Bruce Kangwa.
  Triangle FC: Ronald Mudumu, Trevor Mabunga, Donald Dzvinyai, Russel Madamombe, Collis Dhuwa, Timothy January/ Tinashe Anelka Chivandire dk75, Praise Tonha, Obey Mwerahari, Ralph Kawondera, Allan Tavarwisa/ Simba Makoni dk83 na Brian Chikwenya.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YACHAPWA 1-0 NYUMBANI NA TRIANGLE FC YA ZIMBABWE KOMBE LA SHIRIKISHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top