• HABARI MPYA

  Jumapili, Septemba 15, 2019

  KAGERA SUGAR YAENDELEZA UBABE UGENINI LIGI KUU, YAICHAPA ALLIANCE 2-1 NYAMAGANA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Kagera Sugar imeendeleza wimbi la ushindi katika mechi zake za ugenini za Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya leo kuwachapa wenyeji, Alliance FC Uwanja wa Nyamagana mjini Mwanza.
  Lakini haukuwa ushindi mwepesi kwa Kagera Sugar inayofundishwa na Mecky Mexime, kwani ililazimika kutoka nyuma baada ya Alliance FC kutangulia kwa la mshambuliaji wake mkongwe, Jerry Tegete dakika ya 10.
  Kagera Sugar ambayo mechi ya kwanza ilishinda 2-0 dhidi ya Biashara United mjini Musoma, ikasawazisha bao hilo kupitia kwa Evergeristus Mujwahuki dakika ya 20, kabla ya mchezaji wa zamani wa Yanga, Yusuph Mhilu kufunga la ushindi dakika ya 62.

  Mchezo mwingine wa Ligi Kuu leo, Tanzania Prisons wameutumia vyema uwanja wa nyumbani, Sokloine mjini Mbeya kwa kuwachapa Ruvu Shooting 2-1. 
  Mabao ya Prisons yamefungwa na Jumanne Elifadhili dakika ya 15 na Ismail Kada dakika ya 37, wakati la Ruvu limefungwa na Said Dilunga kwa penalti dakika ya 25.
  Nayo Ndanda FC imelazimishwa sare ya 0-0 na Mwadui FC ya Shinyanga katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KAGERA SUGAR YAENDELEZA UBABE UGENINI LIGI KUU, YAICHAPA ALLIANCE 2-1 NYAMAGANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top