• HABARI MPYA

  Alhamisi, Septemba 19, 2019

  NGORONGORO HEROES WAENDA UGANDA KUWANIA KOMBE LA CECAFA CHALLENGE U20

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KIKOSI cha timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes kimeondoka leo Dar es Salaam kwenda Uganda kushiriki michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 20 Afrika Mashariki na Kati (CECAFA Challenge U20) inayotarajiwa kuanza Septemba 21 hadi Oktoba 5 mjini Kampala.
  Kikosi hicho kilicho chini ya Kocha Mkuu Zubery Katwila kimeondoka na wachezaji 25 ambao ni makipa; Ally Salim (Simba SC), Razack Shekimweki (Mtibwa Sugar) na Abdul Suleiman aliyepandishwa kutoka timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys.
  Mabeki ni; Oscar Maasai (Azam FC), Andrew Simchiba (Coastal Union), Kibwana Shomari (Mtibwa Sugar), Lusajo Mwaikenda (Azam FC), Dickson Job (Mtibwa Sugar) na Gustapha Simon (Yanga SC).

  Viungo ni Onesmo Mayaya (Mtibwa Sugar), Ally Msengi (KMC), Kelvin Nashon (JKT), Wilbroard Maseke (Azam FC), Gadafi Said (Azam FC) na Novatus Dissmas (Biashara United).
  Washambuliaji ni Kelvin John (Huru), Frank Kahole (Mtibwa Sugar), Tepso Evance (Azam FC), Israel Mwenda (Alliance FC), Kassim Shaaban (Sahare FC) na Said Luyeye (JKT Tanzania).
  Ngorongoro imepangwa Kundi B pamoja na Kenya, Ethiopia na Zanzibar, wakati Kundi A litakuwa na wenyeji, Uganda, Sudan, Eritrea na Djibouti na Kundi B linazikutanisha timu za Burundi, Sudan Kusini Somali. 
  Ngorongoro Heroes itafungua dimba na Ethiopia Septemba 22, kabla ya kumenyana na Kenya Septemba 24 na kumaliza mechi zake za Kundi B kwa kupambana na ndugu zao, Zanzibar Septemba 26.
  Hatua ya Robo Fainali itafuatia Septemba 29, Nusu Fainali Okatoba 2 na Fainali ya michuano ya CECAFA Challenge U20 mwaka 2019 itapigwa Oktoba 5.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NGORONGORO HEROES WAENDA UGANDA KUWANIA KOMBE LA CECAFA CHALLENGE U20 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top