• HABARI MPYA

  Ijumaa, Septemba 27, 2019

  PETRO DE LUANDA YA KWANZA KUTINGA MAKUNDI LIGI YA MABINGWA

  MABINGWA wa Angola, Petro de Luanda wamekuwa timu ya kwanza kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuitoa timu ya Mamlaka ya Jiji la Kampala (KCCA).
  Petro de Luanda wamefuzu kwa faida ya mabao ya ugeninibaada ya sare ya 1-1 na KCCA leo Uwanja wa Lugogo mjin Kampala.
  Na hiyo ni baada ya sare ya 0-0 kwenye mchezo wa kwanza mjini Luanda wiki mbili zilizopita.

  Katika mchezo wa leo, Petro de Luanda walitangulia kwa bao la Ricardo Estevao dakika ya 34 kwa penalti iliyotolewa baada ya kipa wa KCCA, Charles Lukwago kumchezea rafu, Isaac Mensah ndani ya boksi.
  Pamoja na hayo, KCCA ikapambana na kipindi cha pili na kufanikiwa kusawazisha kupitia kwa Mustafa Kizza aliyemalizia kazi nzuri ya Sadat Anaku dakika ya 57. 
  Sasa KCCA watamenyana na moja ya timu zilizovuka Raundi ya Pili ya Kombe la Shirikisho kuwania kucheza hatua ya makundi ya michuano hiyo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: PETRO DE LUANDA YA KWANZA KUTINGA MAKUNDI LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top