• HABARI MPYA

  Jumamosi, Septemba 21, 2019

  KAGERA SUGAR YAENDELEZA WIMBI LA USHINDI LIGI KUU, MTIBWA MECHI TATU SASA BILA USHINDI

  Na Mwandishi Wetu, MWANZA
  TIMU ya Kagera Sugar imeendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya leo kuwachapa wenyeji, Mbao FC 1-0 Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.
  Nyota wa mchezo wa leo ni kiungo Awesu Awesu aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 38, kikosi cha kocha Mecky Mexime kikishinda mechi ya tatu mfululizo na zote ugenini.
  Hiyo ni baada ya kushinda 2-0 dhidi ya Biashara United Uwanja wa Karume mjini Musoma kabla ya kuwapiga 2-1 Alliance FC Uwanja wa Nyamagana hapo hapo Mwanza kwenye mechi zake mbilo zilizopita. 

  Mechi nyingine ya Ligi Kuu, Bao la mshambuliaji mkongwe, Hussein Javu liliwanusuru wenyeji Ndanda SC kuchapwa na Singida United nyumbani Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara kufuatia Frank Zakaria kuanza kuwafungia wageni dakika ya tano.
  Nayo Mbeya City imetoa sare ya 1-1 na Ruvu Shooting katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu leo, Peter Mapunda akianza kuwafungia wenyeji dakika ya 18 Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya kabla ya George Chota kujifunga dakika ya 37 kuwapa wageni bao la kusawazisha.
  Mechi nyingine mbili za Ligi Kuu leo zote zimemalizika kwa sare za bila mabao, JKT Tanzania na Mtibwa Sugar Uwanja wa Meja Isamuhyo na Namungo FC dhidi ya Mwadui FC Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KAGERA SUGAR YAENDELEZA WIMBI LA USHINDI LIGI KUU, MTIBWA MECHI TATU SASA BILA USHINDI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top