• HABARI MPYA

  Jumapili, Septemba 15, 2019

  KOCHA WA ZAMANI WA TAIFA STARS RUDI GUTENDORF AFARIKI DUNIA KWAO UJERUMANI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KOCHA wa zamani wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars Mjerumani Rudolf ‘Rudi’ Gutendorf  amefariki dunia akiwa ana umri wa miaka 93 jana.
  Taarifa ya familia yake nchini Ujerumani imesema kwamba Gutendorf aliyeweka rekodi ya dunia ya kufundisha timu nyingi zaidi duniani, 55 katika nchi 32 za mabara matano amefariki dunia jana.
  Makamu wa Rais wa Chama cha Soka Ujerumani, Dk Rainer Koch alimpe heshima ya “Balozi Bora wa Soka ya Ujerumani”.
  Baada ya kuichezea klabu ya TuS Neuendorf ya kwao, Ujerumani tangu mwaka 1944 kama kiungo mshambuliaji, Gutendorf alistaafu mwaka 1953 na kwenda kupata kozi ya ukocha chini ya Sepp Herberger.
  Alipata leseni ya ukocha mwaka 1954 na kuanza safari yake ya kufundisha timu 55 katika nchi 32 za mabara matano duniani, ikiwemo Tanzania.
  Kwa mara ya mwisho Gutendorf alifundisha kikosi cha timu ya taifa ya Samoa mwaka 2003 baada ya kuweka pia rekodi ya kuwa kocha wa kwanza wa kigeni kutwaa taji la Ligi Kuu ya Japan mwaka 1984 akiwa na klabu ya Yomiuri SC.
  Nchini Tanzania atakumbukwa zaidi alipoiwezesha Bara kufika fainali ya michuano hiyo mwaka 1981  mjini Dar es Salaam na kufungwa na Kenya Novemba 28, bao pekee la James Ouma dakika ya 22.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KOCHA WA ZAMANI WA TAIFA STARS RUDI GUTENDORF AFARIKI DUNIA KWAO UJERUMANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top