• HABARI MPYA

  Alhamisi, Septemba 19, 2019

  MSHAMBULIAJI MBRAZIL WA SIMBA SC, WILKER DA SILVA SASA YUKO FITI KUANZA KAZI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI Mbrazil, Wilker Henrique da Silva aliyekuwa majeruhi ameanza mazoezi Simba SC baada ya kupona maumivu yaliyokuwa yanamsumbua.
  Taarifa ya SImba SC imesema kwama Silva mwenye umri wa miaka 23 amepona na sasa yupo tayari kuwatumikia na kuwapa furaha wapenzi wa timu hiyo.
  Silva aliyesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na klabu bingwa ya Tanzania Bara, Simba SC Julai mwaka huu akitokea klabu ya Bragantino inayocheza Ligi Daraja la Nne nchini kwao, Brazil hajaichezea timu hiyo hata mechi moja.
  Kocha Mbelgiji wa Simba SC, Patrick Aussems akimuongoza mshambuliaji Mbrazil, Wilker Henrique da Silva mazoezi  

  Wilker Henrique da Silva akimtoka kiungo Msudan, Sharaf Eldin Shiboub mazoezini Simba SC  

  Lakini Wabrazil wengine wawili waliosajiliwa Simba SC msimu huu, mabeki Tairone Santos da Silva mwenye umri wa miaka 30 na Gerson Fraga Vieira mwenye umri wa miaka 26 anayeweza kucheza kama kiungo wa ulinzi pia wamekwishaanza kutumika.
  Kwa upande wake, Tairone Santos da Silva alitokea klabu ya Atletico Cearense FC inayocheza Ligi Daraja la Nne nchini Brazil, maarufu kama Serie D na Gerson Fraga Vieira ametoka ATK ya Ligi Kuu ya India.
  Wilker Henrique da Silva amekuwa mchezaji wa Bragantino tangu mwaka 2015 alipojiunga nayo kutoka Ponte Preta, ingawa mwaka 2018 alikwenda kuichezea Uniao Barbarense iliyokuwa Daraja la tatu kabla ya kurejea timu yake hiyo hadi Julai alipotua Msimbazi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MSHAMBULIAJI MBRAZIL WA SIMBA SC, WILKER DA SILVA SASA YUKO FITI KUANZA KAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top