• HABARI MPYA

  Ijumaa, Septemba 20, 2019

  TIGO NA SPORTPESA WAZINDUA PROMOSHENI YA FAIDIKA NA JERO, AMBAYO WATEJA WATAJISHINDIA ZAWADI KABAMBE

  Na Asha Said, DAR ES SALAAM
  KAMPUNI ya simu za mkononi ya Tigo Tanzania leo imeingia kwenye ushirikiano na SportPesa Tanzania kwa kuzindua promosheni kabambe ambapo wateja wa Tigo watajishindia zawadi wanapobashiri mara baada ya kuweka pesa kwenye akaunti ya SportPesa kupitia Tigo Pesa.
  Kupitia FAIDIKA NA JERO, wateja wataweza kujishinda zawadi aina ya smartphone kila siku wakati kwenye droo ya mwisho mteja mmoja atajishindia gari mpya Renault Kwid kwa kubashiri kuanzia kiasi cha Tshs 500 tu.
  Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kuzindua promosheni hiyo, Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti SportPesa Tanzania Tarimba Abbas alisema “Kupitia vyombo vya habari tutatangaza washindi wa kila wiki na atakabidhiwa zawadi yake bila gharama yoyote,”.
  Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti SportPesa Tanzania, Tarimba Abbas (kushoto) akiwa na wachezaji wa Simba na Yanga katika uzinduzi wa Promosheni hiyo leo Dar es Salaam. Kulia ni Meneja Uhusiano Tigo Tanzania Woinde Shisael  
  Meneja Uhusiano SportPesa, Sabrina Msuya (kulia) akizungumza kwenye uzinduzi wa promosheni ya Faidika na Jero leo

  “Mteja atatakiwa kujisajili, kuweka fedha kwenye akaunti ya SportPesa kupitia mtandao wa tigo, kucheza na SportPesa ili ashinde’. “Naomba nitoe rai kwa wateja wa Tigo kutumia fursa hii na kuanza kubashiri na kupata nafasi ya kujishindia simu mpya aina ya Samsung A10s au gari mpya kwenye droo kubwa ya mwisho’”, alisema Tarimba.
  Droo za promosheni zitakuwa zikichezezwa kila Jumatano kwa washindi wa simu huku droo ya mwisho ikiwa na zawadi ya gari aina ya Renault Kwid ambayo ina matumizi mazuri ya mafuta km23/lita ya mafuta.
  Kwa upande wake, Meneja Uhusiano Tigo Tanzania Woinde Shisael alisema, ‘Hii ni fursa nyingine kwa Tigo kuwazawadia wateja kupitia promosheni hii ya FAIDIKA NA JERO. ‘Tigo imekuwa ikizindua bidhaa na huduma zenye ubunifu wa hali ya juu na zinazokidhi matakwa ya wateja wetu.
  “Tunaelewa ni njisi gani wateja wetu wanapenda michezo na ni sehemu ya maisha. Kwa kupitia ushirikiano wetu huu na SportPesa, tunawapa wateja wetu fursa ya kujishindia zawadi kwa kubashiri na kuweka pesa kupitia Tigo Pesa,”.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TIGO NA SPORTPESA WAZINDUA PROMOSHENI YA FAIDIKA NA JERO, AMBAYO WATEJA WATAJISHINDIA ZAWADI KABAMBE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top