• HABARI MPYA

  Jumamosi, Septemba 14, 2019

  NAMUNGO FC YAENDELEZA WIMBI LA USHINDI LIGI KUU, YAICHAPA SINGIDA UNITED 2-0 MAJALIWA

  Na Mwandishi Wetu, RUANGWA
  TIMU ya Namungo FC imeendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya leo kuichapa Singida United 2-0 katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.
  Ushindi huo wa timu hiyo iliyopanda Ligi Kuu msimu huu umetokana na mabao ya mshambuliaji Reliant Lusajo dakika ya 27 na kiungo Mohamed ‘Mo’ Ibrahim dakika ya 46.
  Mchezo mwingine wa Ligi Kuu leo, Mbao FC imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya majirani, Biashara United bao pekee la Emmanuel Lukinda dakika ya 21 Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.


  Na Lipuli FC wakaendeleza wimbi la ushindi wakiwachapa wenyeji, JKT Tanzania 1-0 Uwanja wa Meja Isamuhyo huko Mbweni, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
  Ligi Kuu itaendelea kesho kwa mechi tatu Ndanda FC wakiwakaribisha Mwadui FC Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara, Tanzania Prisons wakiwa wenyeji wa Ruvu Shooting Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya na Alliance FC wakimenyana na Kagera Sugar FC Uwanja wa Nyamagana mjini Mwanza.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NAMUNGO FC YAENDELEZA WIMBI LA USHINDI LIGI KUU, YAICHAPA SINGIDA UNITED 2-0 MAJALIWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top