• HABARI MPYA

  Jumapili, Septemba 22, 2019

  DOGO WA AZAM AKADEMI APIGA HAT TRICK TANZANIA BARA YAICHAPA ETHIOPIA 4-0 UGANDA

  Na Mwandishi Wetu, JINJA
  TANZANIA Bara imeanza vyema michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 20 Afrika Mashariki na Kati (CECAFA Challenge U20) baada ya ushindi wa 4-0 dhidi ya Ethiopia leo mjini Jinja, Uganda.
  Nyota wa mchezo wa leo alikuwa ni chipukizi wa akademi ya Azam FC aliyekuwa kwa mkopo Coastal Union ya Tanga, Andrew Albert Simchimba aliyefunga mabao matatu peke yake dakika za 38, 49 na 85, baada ya chipukizi mwingine, Kelvin Pius John aliye mbioni kusajiliwa KRC Genk ya Ubelgiji kufunga la kwanza dakika ya 18.
  Bara inayofundishwa na kocha wa Mtibwa Sugar ya Morogoro, Zubery Katwila itarudi uwanjani Jumanne kumenyana na Kenya kabla ya kukamilisha mechi zake za Kundi B kwa kucheza na ndugu zao, Zanzibar Septemba 26.
  Chipukizi Andrew Simchiba akishangilia na wenzake baada ya kuifungia Bara mabao matatu leo

  Mfungaji wa bao la kwanza la Bara, Kelvin Pius John (kulia) akiwania mpira dhidi ya beki wa Ethiopia

  Hatua ya Robo Fainali itafuatia Septemba 29, Nusu Fainali Okatoba 2 na Fainali ya michuano ya CECAFA Challenge U20 mwaka 2019 itapigwa Oktoba 5.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: DOGO WA AZAM AKADEMI APIGA HAT TRICK TANZANIA BARA YAICHAPA ETHIOPIA 4-0 UGANDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top