• HABARI MPYA

  Jumapili, Septemba 22, 2019

  MBWANA SAMATTA AIONGOZA KRC GENK KUWACHAPA WAPINZANI 3-1 KATIKA LIGI YA UBELGIJI

  Na Mwandishi Wetu, GENK
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta usiku wa jana alikuwa Nahodha wa timu yake, KRC Genk ikiibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya KV Oostende katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk.
  Mabao ya Genk usiku wa jana yalifungwa na kiungo Mvenezuela Ronald Vargas aliyejifunga dakika ya 18, mshambuliaji Mnigeria Ebere Paul Onuachu dakika ya 44 na kiungo Mnorway, Sander Berge dakika ya 90, wakati bao pekee la lilifungwa na mshambuliaj Mguinea, Idrissa Sylla dakika ya 32.
  Ushindi huo katika mchezo wa nane wa msimu, unawafanya KRC Genk, mabingwa watetezi wa ligi hiyo ya Ubelgiji wafikishe pointi 13 sasa wakilingana na AA Gent ambayo hata hivyo imecheza mechi sita na wanaendelea kushika nafasi ya saba.
  Nahodha wa KRC Genk jana, Mbwana Samatta akipiga shuti mbele ya mchezaji wa KV Oostende 
  Nahodha Mbwana Samatta 'Captain Diego' akimpongeza Mnigeria Ebere Paul Onuachu baada ya kufunga jana 

  Genk wanazidiwa pointi mbili na zote, Standard Liege, Antwerp zilizocheza mechi saba na Royal Excel Mouscron iliyocheza mechi nane zinazofuatana nafasi tatu za juu zikifuatiwa na Club Brugge iliyocheza mechi sita na Mechelen mechi nane na zote zina pointi 14 kila moja.
  Samatta mwenye umri wa miaka 26 jana amecheza mechi ya 164 kwenye mashindano yote tangu amejiunga na KRC Genk Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) akiwa amefunga mabao 68 jumla.
  Katika ligi ya Ubelgiji pekee amecheza mechi 129 na kufunga mabao 52, kwenye Kombe la Ubelgiji amecheza mechi tisa na kufunga mabao mawili, katika Super Cup mechi moja, Europa League mechi 24, mabao 14 na Ligi ya Mabingwa mechi moja, bao moja.
  Kikosi cha KRC Genk kilikuwa; Coucke, Maehle, Cuesta, Lucumi, Uronen, Berge, Hrosovsky, Ito, Hagi/Ndongala dk75, Samatta na Onuachu/Heynen dk70.
  KV Oostende; Dutoit, Faes, Milovic, Junior Sakala, Marquet/Jonckheere dk72, Vargas/D'Haese dk65, Skulason, Sylla, Bataille, Vandendriessche na Canesin.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MBWANA SAMATTA AIONGOZA KRC GENK KUWACHAPA WAPINZANI 3-1 KATIKA LIGI YA UBELGIJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top