• HABARI MPYA

  Jumapili, Septemba 15, 2019

  MALINDI SC YACHAPWA 4-1 NA AL MASRY LEO KOMBE LA SHIRIKISHO UWANJA WA AMAAN

  Na Mwandishi Wetu, ZANZIBAR
  TIMU ya Malindi SC leo imeshindwa kutumia vyema fursa ya kucheza nyumbani baada ya kuchapwa mabao 4-1 na Al Masry ya Misri katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Pili ya Kombe la Shirikisho Afrika Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
  Mabao ya Al Masry leo yamefungwa na Mahmoud Wadi mawili dakika ya 27 na 39, Hassan Ibrahim dakika ya 32 na Saidou Simpore dakika ya 52 huku bao pekee la Malindi likifungwa na Ibrahim Ali ‘Imu Mkoko’ dakika ya 42.
  Sasa Malindi SC ambayo ilifika hatua hii baada ya kuitoa Mogadishu City ya Somalia inatakiwa kwenda kushinda 4-0 kwenye mchezo wa marudiano Septemba 27 nchini Misri. 

  Kwa ujumla haikuwa siku nzuri kwa Tanzania, kwani nao wawakilishi wa Bara kwenye michuano hiyo, Azam FC wamefungwa 1-0 na wageni Triangle FC ya Zimbabwe katika mchezo mwingine wa kwanza wa Raundi ya Pili Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam.
  Bao lililoizamisha Azam FC leo limefungwa na Ralph Kawondera dakika ya 35 akimalizia krosi iliyopigwa na Russel Madamombe.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MALINDI SC YACHAPWA 4-1 NA AL MASRY LEO KOMBE LA SHIRIKISHO UWANJA WA AMAAN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top