• HABARI MPYA

  Jumatatu, Machi 27, 2017

  YANGA NA MC ALGER KUCHEZWA MWANZA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MCHEZO wa kwanza wa mchujo wa kuwania hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika baina ya wenyeji, Yanga SC na Mouloudia Club d'Alger, maarufu kama MC Alger ya Algeria ya Algeria huenda ukafanyika Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
  Bin Zubeiry Sports - Online inafahamu kwamba viongozi wa Yanga wapo katika harakati za kufanikisha mpango wa kuuhamishia mchezo huo Mwanza kutoka Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa matarajio ya kupata watazamaji wengi na pato kubwa.
  Tayari mchezo wa Ligi Kuu ya Vodaocm Tanzania Bara kati ya wenyeji Mbao FC na Simba SC ya Dar es Salaam uliokuwa ufanyike Aprili 8, mwaka huu Uwanja wa CCM Kirumba, umesogezwa mbele kwa siku mbili hadi Aprili, 10.
  Lakini taarifa ya Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi, Boniphace Wambura leo imesema kwamba hatua hiyo imechukuliwa ili kupisha shughuli za kijamii kwenye Uwanja huo zitakazoanza Aprili 1 hadi 9.
  Yanga SC imeangukia Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kutolewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa baada ya sare ya 0-0 na wenyeji, Zanaco Uwanja wa Taifa wa Mashujaa, Lusaka nchini Zambia ikitoka kulazimishwa sare ya 1-1 kwenye mchezo wa kwanza Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA NA MC ALGER KUCHEZWA MWANZA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top