• HABARI MPYA

  Alhamisi, Machi 23, 2017

  SAMATTA: STARS INAWEZA KUTUSUA CHINI YA MAYANGA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  NAHODHA wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mbwana Samata amesema kwamba anai mani na Kocha Mkuu mpya wa timu hiyo, Salum Mayanga kwamba anaweza kuiletea mafanikio.
  Mshambuliaji huyo wa KRC Genk, amesema kwamba Mayanga ni kocha mwenye uzoefu kwa sasa na anawajua wachezaji wa Tanzania, hivyo anaweza kufanikiwa.
  Samatta aliyewasili usiku wa juzi kujiunga na kikosi cha Stars kwa ajili ya mechi mbili za kirafiki za kimataifa wiki ijayo dhidi ya Botswana Jumamosi na Burundi Jumanne, amesifu pia uteuzi wa kikosi cha Stars wa Mayanga, kwamba umezingatia makosa yaliyojitokeza kwa walimu waliomtangulia.
  Mbwana Samata amesema kocha mpya wa Taifa Stars, Salum Mayanga anaweza kuiletea mafanikio timu

  Tayari Mayanga amewateua viungo Himid Mao Mkami wa Azam FC na Jonas Gerald Mkude wa Simba, kuwa Manahodha wasaidizi wa timu hiyo, kufuatia aliyekuwa Nahodha Msaidizi na Nahodha wa kikosi cha wachezaji wa nyumbani, John Raphael Bocco ‘Adebayor’ kuwa majeruhi tangu Januari mwaka huu.
  Taifa Stars inatarajiwa kucheza mechi mbili, kwanza na Botswana Machi 25 na baadaye Burundi Machi 28, mwaka huu Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam na pamoja na Samatta, mchezaji mwingine wa Tanzania anayecheza Ulaya, Farid Mussa wa Tenerife ya Hispania anatarajiwa pia kuwasili kesho.
  Kikosi kamili cha Stars kwa ajili ya mechi hizo kilichopo kambini hoteli ya Urban Rose, Dar es Salaam kinaundwa na makipa; Aishi Manula (Azam FC), Deogratius Munishi (Yanga SC) na Said Mohammed (Mtibwa Sugar).
  Walinzi wa pembeni upande wa kulia aliwataja Shomari Kapombe (Azam FC) na Hassan Kessy (Yanga SC) wakati upande wa kushoto wapo Mohammed Hussein (Simba) na Gadiel Michael (Azam FC).
  Walinzi wa kati Vicent Andrew (Yanga SC), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Abdi Banda (Simba SC) na Erasto Nyoni (Azam FC) ilihali aliwataja viungo wa kuzuia kuwa ni Himid Mao (Azam FC) na Jonas Mkude (Simba SC).
  Kadhalika wako viungo wa kushambulia Salum Abubakar (Azam FC), Said Ndemla (Simba SC), Frank Domoyo (Azam FC) na Muzamil Yassin (Simba) wakati viungo wa kulia waliotajwa ni Simon Msuva (Yanga SC) na Shizza Kichuya (Simba SC).
  Viungo wa kushoto ni Farid Mussa (Teneriffe, Hispania) na Hassan Kabunda (Mwadui FC) wakati washambuliaji ni Samatta (KRC Genk- Ubelgiji), Ibrahim Hajib (Simba SC), Mbaraka Yussuf (Kagera Sugar) na Abdul-Rahman Mussa (Ruvu Shooting).
  Mayanga anasaidiwa kocha wa Makipa, Patrick Mwangata; Meneja wa timu, Danny Msangi; Mtunza Vifaa, Ally Ruvu wakati Daktari wa timuatakuwa Richard Yomba huku Daktari wa viungo akiwa ni Gilbert Kigadya.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SAMATTA: STARS INAWEZA KUTUSUA CHINI YA MAYANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top