• HABARI MPYA

  Jumapili, Machi 26, 2017

  SAMATTA: PENGO LA ULIMWENGU NJE NJE TAIFA STARS

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  PAMOJA na ushindi wa 2-0 dhidi ya Botswana, Nahodha wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta amesema kwamba mshambuliaji Thomas Emmanuel Ulimwengu ni muhimu katika timu hiyo.
  Taifa Stars jana iliichapa Botswana 2-0 katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam huku Samatta akifunga mabao yote, moja kila kipindi.
  Lakini baada ya mchezo huo, mshambuliaji huyo wa KRC Genk ya Ubelgiji akasema ameliona pengo la Ulimwengu kwenye mchezo huo wa kwanza chini ya kocha Salum Mayanga aliyerithi mikoba ya Charles Boniface Mkwasa. 
  Pengo la Thomas Ulimwengu limeonekana jana Taifa Stars ikiichapa Botswana 2-0 

  “Kitu kingine ni kwamba mimeliona pengo la Ulimwengu, huyu mtu ni muhimu ambaye tumemkosa kwenye mchezo huu kwa sababu ni majeruhi, lakini anahitajika sana kwenye timu,”alisema Samatta kuhusu mchezaji mwenzake huyo wa zamani wa TP Mazembe ya DRC.
  Kwa sasa Ulimwengu anachezea AFC Eskilstuna ya Ligi Kuu ya Sweden na ameshindwa kujiunga na Taifa Stars kwa sababu yuko chini ya uangalizi wa Dakatari nchini humo.
  Nahodha Mbwana Samatta jana alifunga mabao yote dhidi ya Botswana
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SAMATTA: PENGO LA ULIMWENGU NJE NJE TAIFA STARS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top