• HABARI MPYA

  Jumatano, Machi 22, 2017

  MWANJALI SASA TAYARI KUREJEA UWANJANI SIMBA SC

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  BEKI wa kati tegemeo wa Simba, Mzimbabwe Method Mwanjali sasa yu tayari kuanza mazoezi na wenzake baada ya kupata nafuu ya maumivu ya goti.
  Mwanjali hakuwemo kwenye kikosi kilichokwenda Dodoma na Arusha kwenye mechi za kirafiki na Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), au Azam Sports Federation Cup (ASFC) kutokana na maumivu hayo.
  Simba SC ilishinda 3-0 dhidi ya wenyeji, Polisi Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma na 1-0 mara mbili dhidi ya Madini FC Uwanja wa Sheikh Amri Abeid na dhidi ya Mererani Stars Uwanja wa CCM Mererani, Arusha.

  Method Mwanjali aliumia goti katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Prisons Februari 11 


  Na akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online leo, Daktari wa Simba, Yassin Gembe amesema kwamba baada ya timu kurejea kutoka Arusha wanatarajia Mwanjali atarejea kikosini.
  Gembe alisema walitaka Mzimbabwe huyo apumzike kwa mwezi wote wa Machi ili awe fiti zaidi kuliko kumharakisha kurejea uwanjani.
  “Lengo la kumpa mapumziko marefu ni kutaka apone vizuri ndiyo aanze mazoezi, tunaamini kwa sasa atakuwa tayari kabisa,”alisema Gembe. 
  Mwanjali aliumia goti katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Prisons Februari 11, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Simba ikishinda 3-0.
  Mwanjali aliye katika msimu wake wa kwanza Simba SC, alitolewa kwa machela siku hiyo na nafasi yake kuchukuliwa na kiungo Mwinyi Kazimoto dakika ya 62.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MWANJALI SASA TAYARI KUREJEA UWANJANI SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top