• HABARI MPYA

  Alhamisi, Machi 23, 2017

  NAPE APIGWA CHINI WIZARA YA MICHEZO, MWAKYEMBE APEWA MIKOBA

  RAIS wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Dk John Pombe Joseph Magufuli amefanya mabadiliko madogo katika Bara la Mawaziri kwa kumuondoa aliyekuwa Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo, Nape Moses Nnauye na nafasi yake kuchukuliwa na Dk. Harrison Mwakyembe.
  Kabla ya uteuzi huo, Mwakyembe alikuwa Waziri  wa Katiba na Sheria na nafasi yake inajazwa na Profesa Palamagamba Aidan John Mwaluko.
  Taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa imesema kwamba wateule wote wapya wataapishwa kesho mchana Ikulu mjini Dar es Salaam.
  Waziri mpya wa Habari Utamaduni na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NAPE APIGWA CHINI WIZARA YA MICHEZO, MWAKYEMBE APEWA MIKOBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top