• HABARI MPYA

  Ijumaa, Machi 31, 2017

  LUKAKU MCHEZAJI BORA WA MACHI ENGLAND, HOWE KOCHA BORA

  MSHAMBULIAJI wa Everton, Romelu Lukaku ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa mwezi Machi wa Ligi Kuu ya England.
  Lukaku amefunga mabao manne katika mechi tatu mwezi huu, huku pia akisaidia upatikanaji wa mabao mengine mawili na kusiaida The Toffees katika harakani za kuwania kumaliza ndani ya Nne Bora.
  Kocha wa Bournemouth, Eddie Howe ameshinda tuzo ya Meneja bora wa Machi, wakati winga wa Crystal Palace, Andros Townsend ameshinda tuzo ya bao bora la mwezi.
  Romelu Lukaku ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa mwezi Machi wa Ligi Kuu ya England PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

  Lukaku amefunga katika mechi zote tatu za Everton mwezi Machi, moja moja katika ushindi wa 3-2 dhidi ya Tottenham Hotspur na 3-0 dhidi ya West Bromwich Albion, kabla ya kufunga mawili katika ushindi wa 4-0 dhidi ya Hull City.
  Kiwango chake cha sasa kinataka kumuondoa Goodison Park, kufuatia habari za klabu yake ya zamani, Chelsea kutaka kumrejesha Darajani.
  Lukaku sasa ana mabao 21 katika Ligi aliyoifungia timu ya Ronald Koeman msimu huu - anakuwa mchezaji wa kwanza wa Everton kufunga mabao zaidi 20 katika msimu mmoja wa Ligi Kuu England akiwani ufungaji bora msimu huu.
  Akizungumza baada ya kukabidhiwwa tuzo hiyo, Lukaku alisema; :"Inanipa msukumu mwingine. Nacheza vizuri kwa sasa na timu inafanya vizuri,". 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: LUKAKU MCHEZAJI BORA WA MACHI ENGLAND, HOWE KOCHA BORA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top