• HABARI MPYA

    Wednesday, March 29, 2017

    TAMBWE: NIPENI WIKI MOJA NITAKUWA FITI

    Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
    MSHAMBULIAJI tegemeo wa Yanga, Mrundi Amissi Tambwe anahitaji wiki moja zaidi kabla ya kurejea kikamilifu uwanjani, kufuatia kuwa nje kwa muda mrefu kutokana na maumivu ya goti.
    Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online jana, Tambwe alisema kwamba anaamini baada ya wiki moja atakuwa fiti kabisa kuanza mazoezi kikamilifu.
    Alisema kwa sasa anafanya mazoezi mepesi tu katika gym na kukimbia ufukweni ili kuimarika taratibu, lakini kuanzia wiki ijayo anaweza kufanya mazoezi kikamilifu.
    Amissi Tambwe anahitaji wiki moja zaidi kabla ya kurejea kikamilifu uwanjani

    “Bado sijawa fiti kisawasawa, lakini natarajia baada ya wiki moja ndiyo nitakuwa tayari kuanza mazoezi kikamilifu,”alisema.
    Tambwe aliyeumia katika mchezo wa hatua ya 32 Bora ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), au Azam Sports Federation Cup (ASFC) dhidi ya Ashanti United Januari 21 – amekuwa akijaribu mara kadhaa kurejea uwanjani, lakini anajitonesha na kurudi kwenye matibabu.
    Alicheza mechi ya kwanza ya Raundi ya Awali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Ngaya Club nchini Comoro, lakini akashindwa kucheza mechi ya marudiano Dar es Salaam, kabla ya kuibuka kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Simba Februari 25, mwaka huu siku ambayo hakuwa katika ubora wake, Yanga ikifungwa 2-1.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TAMBWE: NIPENI WIKI MOJA NITAKUWA FITI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top