• HABARI MPYA

  Jumapili, Machi 26, 2017

  POGBA WAITWA TIMU YA TAIFA GUINEA KUZIVAA GABON NA CAMEROON

  KAKA zake Paul Pogba’ wawili, Florent na Mathias wote wameitwa kwenye kikosi cha Guinea kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa na dhidi ya Gabon na Cameroon wiki ijayo.
  Katika kujiandaa na mechi za kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika 2019 Juni mwaka huu, Guinea itamenyana na Gabon mjini Le Havre Ijumaa na mabingwa wa Afrikan, Cameroon mjini Brussels, Ubelgiji Alhamisi ijayo.
  Kikosi cha Guinea kimekuwa kikifanya mazoezi mjini Lisses, nje kidogo ya Jiji la Paris, wiki hii chini ya kocha Kanfory Lappe.
  Naby Keita anayecheza Ujerumani ameondolewa kikosini kutokana na kuwa majeruhi, akiungana na Nahodha Ibrahima Traore na mshambuliaji Jose Kante Martinez kuwa nje.
  Paul Pogba na kaka zake hao mwaka 2013 baada ya Juventus kutwaa taji la Serie A 

  Kikosi kamili cha Guinea ni makipa; Abdoul Aziz Keita (AS Kaloum), Thomas Nguettia (Louhans Cuiseaux, Ufaransa), Abdoulaye Sylla (Hafia) na mabeki; Alseny Bangoura, Alsény Camara (wote Horoya), Fode Camara (Hassania Agadir, Morocco), Sekou Conde (Amkar Perm, Russia), Florentin Pogba (St Etienne, Ufaransa), Issiaga Sylla (Toulouse, Ufaransa).
  Viungo ni Ousmane Balde (FK Vereya Stara Zaghora, Bulgaria), Alkhaly Bangoura (Etoile Sahel, Tunisia), Boubacar Fofana (Al Khaleej, Saudi Arabia), Mohamed Mara (Lorient, Ufaransa), Ibrahima Sory Sankhon (Horoya) na washambuliaji Aboubacar Demba Camara (Paris FC, Ufaransa), Lonsana Doumbouya (St. Polten, Austria), François Kamano (Girondins Bordeaux, Ufaransa), Alhassane Keita (Maritimo, Portugal), Mathias Pogba (Sparta Rotterdam, Ufaransa), Seydouba Soumah (Slovan Bratislava, Slovakia).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: POGBA WAITWA TIMU YA TAIFA GUINEA KUZIVAA GABON NA CAMEROON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top