• HABARI MPYA

  Alhamisi, Machi 23, 2017

  MALINZI AMPONGEZA MWAKYEMBE WAZIRI MPYA WA MICHEZO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amempongeza Dk Harrison Mwakyembe kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo.
  Katika taarifa yake fupi kwa vyombo vya Habari leo, Rais Malinzi amesema; “Tunaamini chini ya uongozi wake mahiri Tanzania tutapiga hatua kubwa zaidi katika maendeleo ya michezo. Mola na ambariki na kumuongoza katika kutekeleza majukumu yake,”.
  Rais wa TFF, Jamal Malinzi amempongeza Dk Harrison Mwakyembe kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Michezo

  Mapema leo Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Dk John Pombe Joseph Magufuli amefanya mabadiliko madogo katika Bara la Mawaziri kwa kumuondoa aliyekuwa Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo, Nape Moses Nnauye na nafasi yake kuchukuliwa na Harrison Mwakyembe.
  Kabla ya uteuzi huo, Mwakyembe alikuwa Waziri  wa Katiba na Sheria na nafasi yake inajazwa na Profesa Palamagamba Aidan John Mwaluko.
  Taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa imesema kwamba wateule wote wapya wataapishwa kesho mchana Ikulu mjini Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MALINZI AMPONGEZA MWAKYEMBE WAZIRI MPYA WA MICHEZO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top