• HABARI MPYA

  Jumamosi, Machi 25, 2017

  MAYANGA AMTUPA BENCHI DIDA, AMUANZISHA MANULA STARS NA BOTSWANA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KIPA wa Yanga, Deo Munishi ‘Dida’ ataanzia benchi, wakati Aishi Manula wa Azam FC atasimama langoni katika mchezo dhidi ya Botswana jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar e Salaam katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa.
  Kocha Salum Mayanga amepanga kikosi chake cha kwanza Taifa Stars baada ya kurithi mikoba ya Charles Boniface Mkwasa na amewaanzisha Nahodha Mbwana Samatta kucheza pamoja na chipukizi wa Simba, Ibrahim Hajib katika safu ya ushambuliaji.
  Kocha Salum Mayanga (kushoto) akiwa na Manahodha wake, Mbwana Samatta na Jonas Mkude 

  Kwa ujumla kikosi kiachoanza Taifa Stars leo ni hiki; Aishi Manula, Shomary Kapombe, Mohamed Hussen, Abdi Banda, Erasto Nyoni, Himid Mao, Simon Msuva, Frank Domayo, Mbwana Samatta, Ibrahim Hajib na Shiza Kichuya. 
  Katika benchi wapo Dida, Hassan Kessy, Gadiel Machiel, Vincent Andrew ‘Dante’, Salim Mbonde, Jonas Mkude, Muzamil Yassin, Abubakar Salum ‘Sure Boy’, Farid Mussa, Hassan Kabunda, Abdulhaman Mussa na Mbaraka Yussuf.  Mchezo huo unaanza Saa 10:00 na utarushwa pia moja kwa moja na Azam TV. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAYANGA AMTUPA BENCHI DIDA, AMUANZISHA MANULA STARS NA BOTSWANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top