• HABARI MPYA

  Jumanne, Machi 28, 2017

  YANGA NA PRISONS APRILI 22 ROBO FAINALI KOMBE LA TFF

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  YANGA SC itamenyana na Prisons ya Mbeya Aprili 22, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika Robo Fainali ya mwisho ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC).
  Taarifa kutoka TFF zimesema kwamba michezo miwili ya mwisho ya Robo Fainali za ASFC zimepangiwa tarehe na pazia la nane bora litafungwa Aprili 22.
  Mbali na mchezo kati ya Yanga na Prisons, Azam FC wataikaribisha Ndanda FC ya Mtwara Aprili 5, mwaka huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam kuanzia Saa 1:00 usiku.
  Nyota wa Yanga SC, Simon Msuva ana jukumu la kuibeba timu yake mbele ya Prisons

  Tayari Simba ya Dar es Salaam na Mbao FC ya Mwanza zimekwishafuzu hatua ya Nusu Fainali baada ya kuzitoa Kagera Sugar ya Bukoba na Madini FC ya Arusha katika Robo Fainali.
  Mbao FC iliwafunga Kagera Sugar 2-1 Uwanja wa Kaitaba, Bukoba wakati Simba SC iliwafunga Madini FC 1-0 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha bao pekee la Mrundi, Laudit Mavugo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA NA PRISONS APRILI 22 ROBO FAINALI KOMBE LA TFF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top