• HABARI MPYA

  Jumanne, Machi 28, 2017

  SAMATTA AREJEA UBELGIJI, KUWAKOSA BURUNDI LEO

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  NAHODHA wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars Mbwana Samatta ameondoka kurejea Ubelgiji na hatakuwepo kwenye kikosi kitakachomenyana na Burundi leo jioni Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 
  Samatta aliyefunga mabao yote katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Botswana Jumamosi, amelazimika kurejea ili kuwahi maandalizi ya klabu yake kwa mchezo wa Robo Fainali ya UEFA Europa League dhidi ya Celta de Vigo nchini Hispania Aprili 13.
  Mbwana Samatta atakosekana leo kwenye mchezo dhidi ya Burundi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

  Kwa kumkosa Samatta, kocha wa Taifa Stars, Salum Mayanga amemuanzisha Ibrahim Hajib kama mshambuliaji kiongozi akicheza na kiungo Farid Mussa, huku pembeni akiwatumia kiungo Muzamil Yassin kulia na winga Simon Msuva kushoto.
  Kwa ujumla kikosi cha Stars leo kipo hivi; Deo Munishi ‘Dida’, Shomary Kapombe, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Abdi Banda, Salim Mbonde, Himid Mao, Muzamil Yassin, Salum Abubakr ‘Sure Boy’, Ibrahim Hajib, Farid Mussa na Simon Msuva.
  Katika benchi watakuwapo Said Mohammed, Hassan Kessy, Gareiel Michael, Hassan Kabunda, Jonas Mkude, Mbarak Yussuf, Abdulrahman Juma, Shiza Kichuya na Frank Domayo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SAMATTA AREJEA UBELGIJI, KUWAKOSA BURUNDI LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top