• HABARI MPYA

  Jumatatu, Machi 27, 2017

  TIMU YA RAIS MPYA WA CAF YAFUZU MAKUNDI KUFUZU AFCON

  TIMU ya Ahmad, rais mpya wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Madagascar imefuzu hatua ya makundi ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Cameroon mwaka 2019 baada ya ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Sao Tome & Principe jana mjini Antananarivo.
  Matokeo hiyo yanakifanya kisiwa hicho kisonge mbele kwa ushindi wa jumla wa 4-2 baada ya kushinda 1-0 katika mchezo wa kwanza Jumatano. 
  ‘Les Barea’ ilipata bao la kuongoza sekunde ya 60 kupitia kwa Paulin Voavy, ambaye alifunga na la pili dakika ya 17.
  Rais mpya wa CAF, Ahmad (katikati) timu yake imefuzu hatua ya makundi

  Harramiz Ferreira Soares akawafungia Sao Tome bao moja dakika ya 28, kabla ya Carolus Andriamahitsinoro kuifungia Madagascar dakika ya 81 na Jose da Silva Varela kuiongezea bao Tome dakika ya 84.
  Madagascar sasa inaingia Kundi A kuungana na Senegal, Equatorial Guinea na Sudan, wakati nafasi nyingine mbili zitapata washiriki leo baada ya mechi kati ya Mauritius na Comoros na Sudan Kusini dhidi ya Djibouti.
  Wakati huo huo: Katibu Mkuu wa CAF, Mmorocco, Hicham el Amrani mwenye umri wa miaka 38, amejiuzulu jana kwa kuwasilisha barua baada ya uongozi mpya kuingia madarakani.
  Amrani anaondoka ofisi za CAF, Cairo nchini Misri baada ya miaka nane ya kufanya kazi chini ya Rais Mcameroon, Issa Hayatou aliyeshindwa na Ahmad katika uchaguzi.
  Amrani na Hayatou wapo chini ya uchunguzi juu ya mauzo ya haki za Televisheni kwa kampuni ya Kifaransa, Lagardere.
  Ratiba na matokeo mechi za awali
  Jumapili Machi 26, 2017
  Madagascar 3-2 Sao Tome & Principe (1-0)
  Jumanne Machi 28, 2017
  Mauritius vs Comoros (0-2)
  Sudan Kusini vs Djibouti (0-2)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TIMU YA RAIS MPYA WA CAF YAFUZU MAKUNDI KUFUZU AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top