• HABARI MPYA

    Wednesday, March 22, 2017

    YANGA ITAWAKOSA NGOMA NA TAMBWE DHIDI YA AZAM

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    YANGA SC haina matumaini ya kuwapata washambuliaji wake tegemeo, Amissi Tambwe na Donald Ngoma kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Azam FC Aprili 1, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh amesema leo katika mahojiano na Bin Zubeiry Sports – Online kwamba Mrundi Tambwe na Mzimbabwe Ngoma wote majeruhi na labda wanaweza kuanza mazoezi mepesi wiki ijayo.
    Hafidh amesema uwezekano wa wawili hao kuwa tayari kwa ajili ya mchezo dhidi ya Azam Aprili 1 ni mdogo mno, kwa sababu bado wanasumbuliwa na maumivu.
    Amissi Tambwe atakosekana kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Azam FC Aprili 1, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

    “Wote wanaendelea na matibabu, wakati tunakwenda Zambia walipewa wiki mbili za mapumziko, maana yake wana moja zaidi ya kuendelea kuwa nje. Hivyo kuwatarajia kuwa tayari kucheza wiki ijayo ni vigumu,”amesema Hafidh.
    Wawili hao wote wamekuwa wakisumbuliwa na maumivu, Tambwe goti na Ngoma kifundo cha mguu baada ya kuumia kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi, visiwani Zanzibar.
    Pamoja na hayo, kutokana na umuhimu wao katika klabu na pia kukosekana kwa washambuliaji wengine walio tayari, wachezaji wote hao wamewahi kutumika kwa kulazimishwa kabla ya maamuzi ya kupumzishwa wiki iliyopita.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA ITAWAKOSA NGOMA NA TAMBWE DHIDI YA AZAM Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top