• HABARI MPYA

  Jumatano, Machi 22, 2017

  MARC WILMOTS SASA NDIYE KOCHA MPYA IVORY COAST

  KOCHA wa zamani wa Ubelgiji, Marc Wilmots ameteuliwa kuiongoza Ivory Coast katika mechi za kufuzu Kombe la Dunia, Mamlaka ya soka nchini humo imesema jana.
  Wilmots, mwenye umri wa miaka 48, ni miongoni mwa wachezaji waliong’ara akicheza fainali nne za Kombe la Dunia na kuiongoza Ubelgiji katika Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014 katika kipindi cha kati ya 2012 na 2016 alipoiongoza timu hiyo. 
  Moja ya timu tishio Afrika na zenye desturi ya kufuzu Kombe la Dunia, Ivory Coast iliporomoka vibaya ilipokwenda kutetea Kombe la Mataifa ya Afrika mapema mwaka huu baada ya kutolewa raundi ya Kwanza tu nchini Gabon.
  Kwa matokeo hayo, kocha Mfaransa, Michel Dussuyer akafukuzwa na nafasi yake akakaimu Ibrahim Kamara, ambaye wiki iliyopita alifanya mabadiliko makubwa katika kikosi alichoteua kwa ajili ya michezo ya kirafiki dhidi ya Urusi na Senegal.
  Tembo hao wanaongoza Kundi C kwa pointi zao nne walizovuna kwenye mechi mbili kuelekea mechi mbili mbili na Morocco na Gabon na moja na Mali wakihitaji matokeo mazuri ili kukata tiketi ya Urusi mwaka 2018.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MARC WILMOTS SASA NDIYE KOCHA MPYA IVORY COAST Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top