• HABARI MPYA

    Wednesday, March 22, 2017

    WACHEZAJI WANNE WASIMAMISHWA MAJI MAJI

    Na Mwandishi Wetu, SONGEA
    WACHEZAJI wanne wa Maji Maji ya Songea mkoani Ruvuma, George Mpole, Peter Joseph, Yussuf Mfanyaje na Ibrahim Tende wamesimamishwa kwa tuhuma za utovu wa nidhamu.
    Mwenyekiti wa Wana Lizombe hao, Humphrey Milanzi amesema kwamba wachezaji hao wamefanya utovu wa nidhamu ambao klabu haiwezi kuuvumilia.
    Milanzi amesema kwamba ili liwe fundisho kwa wachezaji wengine, uongozi umeamua kuwasimamisha wachezaji hao.
    Na amesema wachezaji hao wanaweza kusamehewa iwapo tu watajirekebisha na kuomba msamaha kutokana na makosa yao.
    Aidha, Milanzi alisema kwamba kwa sasa uongozi unajikita katika jitihada za kuhakikisha unainusuru timu kushuka Daraja kwa kuhakikisha timu inashinda mechi zake zote saba zilizosalia za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.  
    Maji Maji kwa sasa inashika nafasi ya pili kutoka mwisho katika msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 22 baada ya kucheza mechi 24, juu ya JKT Ruvu inayoshika mkia kwa pointi zake 20 za mechi 24 pia.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WACHEZAJI WANNE WASIMAMISHWA MAJI MAJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top