• HABARI MPYA

  Jumatatu, Machi 27, 2017

  TAMBWE AANZA KUJIFUA GYM, LEO JIONI ATAKUWA UWANJANI

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI tegemeo wa Yanga, Mrundi Amissi Tambwe leo ameanza mazoezi mepesi kujaribu kurejea uwanjani baada ya kuwa nje tangu Februari 25, mwaka huu kwa maumivu ya goti.
  Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online leo mjini Dar es Salaam, Tambwe amesema kwamba juzi alianza mazoezi mepesi ya gym na jioni ya leo anatarajia kuanza mazoezi mepesi ya kukimbia uwanjani.
  “Nimeanza mazoezi mepesi ya gym, lakini leo jioni ninatarajia kuhamia uwanjani ambako wenzangu wanafanya kufanya mazoezi mepesi ya kukimbia kimbia pia,”amesema Tambwe.
  Amissi Tambwe leo ameanza mazoezi mepesi kujaribu kurejea uwanjani baada ya kuwa nje tangu Februari 25, mwaka huu kwa maumivu ya goti

  Kimsingi Tambwe ni majeruhi tangu mapema Janauri baada ya kuumia kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar, lakini amekuwa akijaribu mara kadhaa kurudi uwanjani bila mafanikio.
  Februari 25 mwaka huu alianzishwa kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam dhidi ya mahasimu Simba SC, lakini hakuwa na madhara Yanga ikifungwa 2-1 licha ya wapinzani kucheza pungufu karibu kipindi chote cha pili, baada ya beki Mkongo, Janvier Bokungu kutolewa kwa kadi nyekundu. 
  Yanga ipo katika kipindi kigumu kwa sasa, kwani hata mshambuliaji wake mwingine tegemeo, Mzimbabwe Donald Ngoma ni majeruhi kuelekea mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Azam FC Aprili 1, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TAMBWE AANZA KUJIFUA GYM, LEO JIONI ATAKUWA UWANJANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top