• HABARI MPYA

  Jumapili, Machi 26, 2017

  MAVUGO KUIONGOZA BURUNDI DHIDI YA STARS JUMANNE

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI nyota wa Simba SC, Laudit Mavugo ataiongoza Burundi katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya wenyeji, Tanzania Jumanne Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Kikosi cha Int’hamba Murugamba kimewasili mchana wa leo Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo huo wa kirafiki Jumanne na bahati mbaya kitamkosa mshambuliaji mwingine anayecheza Tanzania, Amissi Tambwe wa Yanga ambaye ni majeruhi.
  Ofisa wa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas amesema kwamba Burundi imefikia hoteli ya De Mag, iliyopo Mwananyamala, Dar es Salaam.
  Laudit Mavugo ataiongoza Burundi katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Taifa Stars Jumanne

  “Wageni wetu Burundi wamewasili salama Dar es Salaam tayari kabisa kwa mchezo wa keshokutwa na leo watafanya mazoezi Uwanja wa Karume,”amesema Lucas.
  Msemaji huyo wa TFF, ameongeza kwamba kesho Saa 5:00 kutakuwa na Mkutano na Waandishi wa Habari katika hoteli ya Urban Rose, eneo la Kisutu, Dar es Salaam kuuzungumzia mchezo huo.
  Taifa Stars itaingia kwenye mchezo huo ikitoka kuifunga Botswana 2-0 jana Uwanja wa Taifa, Nahodha Mbwana Samatta akifunga mabao yote.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAVUGO KUIONGOZA BURUNDI DHIDI YA STARS JUMANNE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top