• HABARI MPYA

    Thursday, March 30, 2017

    MAREFA WA RWANDA, GUINEA KUCHEZESHA YANGA NA WAALGERIA

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    SHIRIKISHO ya Soka Afrika (CAF), limewateua marefa wa Rwanda na Guinea kuchezesha mechi mbili za mchujo wa kuwania kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Yanga SC na MC Alger ya Algeria.
    Mchezo wa kwanza Aprili 8, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam utachezeshwa na Louis Hakizimana Atakayepuliza Filimbi Akisaidiwa Na Theogene Ndagijimana na Jean Bosco Niyitegeka wote kutoka Rwanda.
    Mchezo wa marudiano Aprili 14 nchini Algeria utachezeshwa na marefa wa Guinea, ambao ni Yakhouba Keita, Aboubacar Doumbouya na Mamady Tere na mshindi wa jumla atafuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika mwaka huu.
    Mwaka jana pia Yanga ilitolewa katika Ligi ya Mabingwa na kuangukia kwenye kapu la kuwania hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho ambako ilifuzu baada ya kuitoa Sagrada Esperanca ya Angola. 
    Yanga SC imeangukia Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kutolewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa baada ya sare ya 0-0 na wenyeji, Zanaco Uwanja wa Taifa wa Mashujaa, Lusaka nchini Zambia ikitoka kulazimishwa sare ya 1-1 kwenye mchezo wa kwanza Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAREFA WA RWANDA, GUINEA KUCHEZESHA YANGA NA WAALGERIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top