• HABARI MPYA

    Wednesday, March 29, 2017

    CAF YAIGOMEA YANGA KUPELEKA MECHI NA WAARABU KIRUMBA

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    SHIRIKISHO ya Soka Afrika (CAF), limekataa mchezo wa kwanza wa mchujo wa kuwania kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Yanga SC na MC Alger ya Algeria kuchezwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza Aprili 8, mwaka huu kutokana na wenyeji kuchelewesha kuthibitisha mabadiliko ya Uwanja.
    Uwanja wa nyumbani wa Yanga unaofahamika na waliouthibitisha ni wa Taifa, Dar es Salaam, lakini klabu hiyo ilikuwa katika jitihada za kuuhamishia mchezo huo Mwanza kwa tamaa ya mapato zaidi. 
    Hata hivyo, tarehe ya mwisho ya kuwasilisha mabadiliko yoyote ya Uwanja ilikuwa ni juzi wakati Mkaguzi wa CAF, Maxwell Mtonga kutoka Malawi aliupitisha Uwanja huo jana.
    Mtonga alikuwa Mwanza tangu juzi akiongozwa na Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Salum Madadi katika ukaguzi huo na ameagiza marekebisho madogo madogo.
    CAF imeikatalia Yanga kuuhamishia Mwanza mchezo wake na MC Alger ya Algeria Aprili 8, mwaka huu  

    Meneja wa Uwanja wa CCM Kirumba, Steven Shijja aliahidi kuhakikisha wanafanya marekebisho hayo ndani ya muda kama walivyoelekezwa ili mchezo huo ufanyike Mwanza.
    Na tayari mchezo wa Ligi Kuu ya Vodaocm Tanzania Bara kati ya wenyeji Mbao FC na Simba SC ya Dar es Salaam uliokuwa ufanyike Aprili 8, mwaka huu Uwanja wa CCM Kirumba, ulikwishasogezwa mbele kwa siku mbili hadi Aprili, 10.
    Yanga SC imeangukia Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kutolewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa baada ya sare ya 0-0 na wenyeji, Zanaco Uwanja wa Taifa wa Mashujaa, Lusaka nchini Zambia ikitoka kulazimishwa sare ya 1-1 kwenye mchezo wa kwanza Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Yanga sasa inaweza kucheza Kirumba iwapo tu itafuzu hatua ya makundi na pia watatakiwa kuwasilisha mabadiliko ya Uwanja mapema kwa mujibu wa kanuni.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CAF YAIGOMEA YANGA KUPELEKA MECHI NA WAARABU KIRUMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top