• HABARI MPYA

  Jumanne, Machi 28, 2017

  MAVUGO NA BANDA PATACHIMBIKA TAIFA LEO

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI tegemeo wa Burundi, Laudit Mavugo amesema kwamba anatarajia udhibiti mkali kutoka kwa beki wa Tanania, Abdi Banda wanayecheza naye Simba SC katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa leo jioni Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online jana, Mavugo alisema kwamba anajua Banda ataingia kwa kupania kutaka kuonyesha ubora wake, lakini hahofii hilo atapambana naye kuhakikisha anaisaidia timu yake.
  Laudit Mavugo (kulia) akiichezea Simba SC katika mechi ya Ligi Kuu dhidi ya African Lyon

  “Banda tunacheza naye Simba, ninamjua, ni beki mzuri na kesho najua ataingia amepania kutaka kuonyesha umwamba wake, lakini tutapambana na utakuwa mchezo mzuri kwa sababu timu zote ni nzuri,”alisema.  
  Tanzania itakuwa mwenyeji wa Burundi leo jioni katika mchezo wa pili mfululizo ndani ya siku tatu, ikitoka kuifunga Botswana 2-0 Jumapili Uwanja wa Taifa, mabao yote yakifungwa na Nahodha, Mbwana Samatta.
  Kiingilio cha chini katika mchezo huo kitakuwa Sh. 3,000 kwa majukwaa ya mzunguko wakati viingilio vingine ni Sh. 15,000 kwa VIP A, Sh 10,000 kwa VIP B na VIP C na mchezo huo utaanza Saa 10:30 jioni Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAVUGO NA BANDA PATACHIMBIKA TAIFA LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top