Kiungo wa Azam FC, Frank Domayo akipasua katikati ya wachezaji wa Mbabane Swallows jana Uwanja wa Taifa wa Somhlolo mjini Lobamba, Swaziland katika mchezo wa marudiano hatua ya 32 Bora Kombe la Shirikisho Afrika. Azam ilifungwa 3-0 na kutolewa kwa jumla ya mabao 3-1 baada ya ushindi mwembamba wa 1-0 kwenye mchezo wa kwanza Dar es Salaam
Shaaban Iddi wa Azam akiwatoka wachezaji wa Mbabane Swallows
Winga Ramadhani Singano 'Messi' akipiga mpira katikati ya wachezaji wa Mbabane
Beki wa Azam FC, Eraston Nyoni akiwania mpira wa juu dhidi ya mchezaji wa Mbabane
Beki Shomary Kapombe akimpita beki wa Mbabane
Kikosi cha Azam kabla ya mchezo wa jana na Mbabane Swallows





0 comments:
Post a Comment