• HABARI MPYA

    Wednesday, April 06, 2016

    PIGO AZAM FC, KAPOMBE KUWAKOSA ESPERANCE MECHI ZOTE DAR NA TUNIS

    Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
    HABARI mbaya Azam FC, tena katika wakati mbaya. Beki anayeweza kucheza kama kiungo pia, Shomary Kapombe (pichani kulia) hatacheza mechi zote mbili za Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF) dhidi ya Esperance ya Tunisia.
    Kapombe aliyekosa mechi mbili mfululizo za Ligi Kuu timu hiyo ikitoa sare zote, 1-1 na Toto mjini Mwanza Jumapili na 2-2 na Ndanda leo, Na beki huyo wa zamani wa AC Cannes ya Ufaransa anatarajiwa kusafirishwa kesho kwenda Afrika Kusini kwa matibabu.
    Daktari wa Azam FC, Juma Kwimbe ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE leo kwamba Kapombe hatacheza mechi zote dhidi ya Esperance Jumapili Dar es Salaam na wiki mbili zijazo Tunis kwa sababu ni mgonjwa.
    “Amekuwa akilalamika kuumwa mbavu kiasi cha kulia wakati mwingine, leo ikabidi afanyiwe vipimo na imegundulika anasumbuliwa na Nimonia, hivyo kesho anakwenda Afrika Kusini kwa matibabu,”amesema. 
    Kukosekana kwa Kapombe katika kikosi cha Azam FC wakati huu ambao timu ipo kwenye vita ya kuwania ubingwa wa Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho ni pigo.
    Mbali na kuwa mhimili imara wa safu ya ulinzi, Kapombe pia amekuwa mpishi na mfungaji mzuri wa mabao ya timu msimu huu, hadi sasa akiwa amefunga mabao saba kwenye Ligi Kuu pekee.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PIGO AZAM FC, KAPOMBE KUWAKOSA ESPERANCE MECHI ZOTE DAR NA TUNIS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top