• HABARI MPYA

  Alhamisi, Aprili 28, 2016

  TIGERS WATWAA UBINGWA NAMIBIA BAADA YA MIAKA 31

  KLABU kongwe, Tigers, imemaliza ukame wa miaka 31 wa kusubiri taji Ligi Kuu ya Namibia baada ya kutwaa ubingwa wa msimu wa 2015/2016 wa ligi hiyo.
  Baada ya kulikosakosa mara kadhaa, hatimaye klabu hiyo ya mji Mkuu wa Namibia, imetwaa taji la kwa kishindo huku wamebakiza mechi mbili na kuzima utawala wa Black Africa na African Stars, ambazo zimekuwa zikitawala soka ya Namibia kwa miaka saba iliyopita.

  Tigers licha ya kufungwa 3-2 na Citizens, lakini wamefanikiwa kutwaa ubingwa kwa kufikisha pointi 67, sita zaidi ya Black Africa inayoshika nafasi ya pili katika ligi ya timu 16. Tigers imefungwa mechi tatu tu kati ya 30 msimu huu, ikishinda 20 na sare saba.
  Kwa matokeo hayo, Tigers itaiwakilisha Namibia katika Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TIGERS WATWAA UBINGWA NAMIBIA BAADA YA MIAKA 31 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top