• HABARI MPYA

  Jumatano, Aprili 27, 2016

  SI YANGA TU, HATA AZAM, AU SIMBA NAKIPIGA, ASEMA MCAMEROON WA COASTAL UNION

  Na Somoe Ng’itu, DAR ES SALAAM
  KIUNGO wa Mcameroon wa Coastal Union, Youssoufa Sabo (pichani kulia) amesema kuwa kiwango chake ni cha juu na anastahili kuzichezea timu kongwe za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Azam, Simba au Yanga zote za Dar es Salaam. 
  Sabo aliifunga bao la pekee la Coastal Union katika mechi ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Ranzania (TFF), maarufu kama Kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC) ambayo ilivunjika huku Yanga wakiwa mbele kwa mabao 2-1. 
  Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE Jumapili, Sabo ambaye aliwahi kufanya mazoezi Yanga, lakini Pluijm alimuacha alisema kwamba ameiva na makocha wa timu za ligi kuu Bara wameona uwezo wake. 
  "Najua pale nilipokuja hawakuamini, lakini nashukuru nimewaonyesha mimi nina uwezo gani, niko tayari kuzungumza nao kama wataniita," alisema. 
  Soba akipasua katikati ya viungo wa Yanga, Deus Kaseke (kulia) na Thabani Kamusoko (kushoto)  Hata hivyo, alishangaza Yanga kutolewa katika mapema katika Ligi ya Mabingwa Afrika na Al Ahly, akisema yeye anaweza kujiunga na klabu yoyote watakayokubaliana ili kuitumikia katika msimu ujao. 
  Baada ya mechi kumalizika, Pluijm alimuita Sabo na kuzungumza naye. Hata hivyo Pluijm alikataa kueleza mazungumzo yake na kiungo huyo yalihusu nini. "Siwezi kukwambia tulichokuwa tunazungumza na kuhusu kiwango chake pia siwezi kusema lolote, mimi nilikuwa makini kufuatilia wachezaji wangu tu, ila kumbuka kila mchezaji Tanzania angependa kuchezea Yanga," Pluijm alisema. 
  Sabo pia alifunga bao katika mechi ya robo fainali ya mashindano hayo dhidi ya Simba. Tayari Azam FC imetinga fainali ya mashindano hayo ambayo bingwa wake ataiwakilisha Tanzania Bara katika michuano ya Kombe la Shirikisho (CAF) hapo mwakani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SI YANGA TU, HATA AZAM, AU SIMBA NAKIPIGA, ASEMA MCAMEROON WA COASTAL UNION Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top