• HABARI MPYA

  Jumapili, Aprili 24, 2016

  AZAM YATINGA FAINALI KWA MATUTA

  AZAM FC imetinga Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya kuwafunga wenyeji Mwadui FC kwa penalti 5-3 kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 120 Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga.
  Shujaa wa Azam FC alikuwa ni beki Aggrey Morris, aliyefunga penalti ya tano na kuamsha shangwe kwa wachezaji wenzake.

  Wengine waliofunga penalti za Azam FC ni Nahodha John Bocco, Himid Mao, Allan Wanga na Waziri Salum wakati tatu za Mwadui zilifungwa na Malika Ndeule, Iddi Moby na Jabir Aziz.  Aliyekosa upande wa Mwadui ni Kevin Sabato.
  Dakika 90 za mchezo huo zilimalizika timu hizo zikiwa zimefungana bao 1-1, Azam FC ikitangulia kwa bao la Khamis Mcha ‘Vialli’ dakika ya tatu kabla ya Mwadui kusawazisha kupitia kwa dakika ya 82.
  Katika dakika 30 za nyongeza Azam walitangulia tena kwa bao la Mcha dakika ya 97, kabla ya Jabir Aziz kuisawazishia Mwadui dakika 120.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AZAM YATINGA FAINALI KWA MATUTA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top