• HABARI MPYA

  Jumamosi, Aprili 23, 2016

  SAKHO HATARINI KUFUNGIWA MIEZI SITA KWA KUTUMIA DAWA

  MCHEZAJI wa Liverpool, Mamadou Sakho anakabiliwa na adhabu ya kufungiwa miezi sita baada ya vipimo vya awali kuonyesha anatumia dawa zilizopigwa marufu michezoni za kupunguza unene.
  Hayo yalibainika baada ya mchezo wa marudiano wa Liverpool na Manchester United wa Europa League Machi 17.
  Sakho, mwenye umri wa miaka 26, sasa atafanyiwa vipimo vya pili mapema wiki ijayo ili kuthibitisha kama kweli anatumia dawa hizo - maana yake Sakho anakosa mechi dhidi ya Newcastle United Ligi Kuu ya England leo wakati akisubiri hatima yake.
  Mamadou Sakho (katikati) akiwa jukwaani wakati wa mchezo kati ya Liverpool na Newcastle Uwanja Anfield leo

  Iwapo vipimo vya pili vitakuwa sawa na vya kwanza, Sakho anatarajiwa kupewa adhabu kali. Mchezaji mwenzake wa Liverpool, Kolo Toure alifungiwa miezi sita alipokuwa Manchester City baada ya kugundulika alitumia dawa za kupunguza mwili ambazo alidai alipewa na mkewe. City pia ilipigwa faini ya Pauni 740,000.
  Liverpool kwa sasa wanajiandaa na mchezo wa kwanza wa Nusu Fainali ya Europa League, ambako watakutana na Villarreal nchini Hispania Alhamisi usiku.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SAKHO HATARINI KUFUNGIWA MIEZI SITA KWA KUTUMIA DAWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top